• HABARI MPYA

  Friday, May 10, 2024

  MASAWE APIGA ZOTE MBILI NAMUNGO FC YAILAZA GEITA GOLD 2-0 RUANGWA


  WENYEJI, Namungo FC wameibukana ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na kiungo mkwenye anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, Jacob Raymond Masawe (31) dakika ya 43 na 45'+4.
  Kwa ushindi huo, Namungo FC wanafikisha pointi 30 na kusogea nafasi ya saba, wakizizidi tu wastani wa mabao JKT Tanzania na Kagera Sugar baada ya wote kucheza mechi 26.
  Hali ni mbaya kwa Geita Gold baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao24 za mechi 26 nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja.
  Nyingine mbili, ya 13 na 14 mwisho wa msimu zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASAWE APIGA ZOTE MBILI NAMUNGO FC YAILAZA GEITA GOLD 2-0 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top