• HABARI MPYA

  Saturday, May 25, 2024

  NTIBANZOKIZA AIFUNGIA BAO PEKEE SIMBA YAICHAPA KMC 1-0 ARUSHA

  BAO pekee la kiungo mkongwe, Mrundi Saido Ntibanzokiza dakika ya tatu limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 66, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC na wote wakiwa nyuma ya mabingwa tayari kwa mara ya tatu mfululizo, Yanga wenye pointi 77 baada ya timu zote kucheza mechi 29.
  KMC kwa upande wao baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 39 nafasi ya tano, nyuma ya Coastal Union yenye pointi 42 baada ya wote kucheza mechi 29 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NTIBANZOKIZA AIFUNGIA BAO PEKEE SIMBA YAICHAPA KMC 1-0 ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top