• HABARI MPYA

  Monday, May 13, 2024

  SIMBA SC YAAMBULIA SARE KAITABA, 1-1 NA KAGERA SUGAR


  WENYEJI, Kagera Sugar jana walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Simba SC walitangulia kwa bao la kiungo wa pembeni, Ladack Chasambi dakika ya 24, kabla ya mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 62.
  Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 27 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya saba, wakati Simba SC inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 26 ikibaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenge pointi 60 za mechi 27 na mabingwa watetezi, wenye pointi 68 za mechi 26
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAMBULIA SARE KAITABA, 1-1 NA KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top