• HABARI MPYA

  Friday, May 03, 2024

  SIMBA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 CHAMAZI KOUBLAN AMEWEKA


  WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dares Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na mshambuliaji, Muivory Freddy Michael Koublan dakika ya 35 na kiungo mzawa, Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 64.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 23, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 54 na Yanga 62 baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 17 za mechi 24 nafasi ya mwisho, ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 CHAMAZI KOUBLAN AMEWEKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top