• HABARI MPYA

  Friday, May 24, 2024

  MOTSEPE AHALALISHA BAO LA AZİZ Kİ LILILOKATALIWA MAMELODI NA YANGA PRETORIA


  RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema bao la Yanga lililokataliwa na Refa Dahane Beida wa Mauritania katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Aprili 6, mwaka huu  Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria, Afrika Kusini lilikuwa halali.
  “Baada ya mchezo wa Mamelodi dhidi ya Yanga nilimwambia Rais Karia ‘nilidhani lile ni goli’ kama Rais wa CAF sikutakiwa kusema chochote. Lakini mnajua, na napaswa kuheshemu mchakato na taratibu zote, lakini kama shabiki wa mpira nilivyoangalia niliona ni goli,”.
  “Lakini tunatakiwa kufuata na kuheshimu sheria na VAR lakini nadhani jambo kubwa ni mashabiki kujiamiani tunawahakikishia kuwa Waamuzi, VAR ni ‘WELL CLASS’ na tunahakikisha tumeweka fedha nyingi,” amesema Rais wa CAF, Patrice Motsepe, raia wa Afrika Kusini.
  Yanga SC walitupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns kwa penalti 3-2 kufuatia sare za 0-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Machi 30 na Aprili 6 Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria.
  Lakini katika mchezo wa marudiano Aprili 6 Jijini Pretoria, Refa Dahane Beida wa Mauritania alikataa bao la dakika ya 58 la kiungo mshambuliaji Mburkinabe, Stephane Aziz Ki lililoonekana kudundia ndani ya mstari wa lango.
  Katika mikwaju ya penalti waliofunga za Mamelodi Sundowns walikuwa ni viungo Mchile, Marcelo Allende, Mbrazil Lucas Ribeiro Costa na mzawa, Neo Maema wakati ya nyota kutoka Uruguay, Leandro Sirino iliokolewa na kipa Mmali, Djigui Diarra wa Yanga.
  Waliofunga penalti za Yanga ni winga Mghana, Augustine Okrah na mshambuliaji wa Ivory Coast, Joseph Guédé Gnadou huku Aziz Ki na mabeki Dickson Job na Ibrahim Hamad ‘Bacca’ wakikosa.
  Bahati mbaya kwao, Mamelodi Sundowns walitolewa na Esperance ya Tunisia kwa jumla ya mabao 2-0, ikifungwa 1-0 Rades Aprili 20 na Pretoria Aprili 26.
  Esperance nayo ilitoa sare ya 0-0 na mabingwa watetezi, Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa Fainali Mei 28 Uwanja wa Olimpiki Hammadi Agrebi Jijini Radès na kesho watakuwa ugenini Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
  Al Ahly ilifuzu Robo Fainali kama kınada wa Kundi D ikifuatiwa na Yanga wakizipiku CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOTSEPE AHALALISHA BAO LA AZİZ Kİ LILILOKATALIWA MAMELODI NA YANGA PRETORIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top