• HABARI MPYA

    Monday, April 04, 2022

    SERIKALI YAIPONGEZA SIMBA SC KUTINGA ROBO FAINALI


    WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ameipongeza Simba SC kwa kufuzu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibamiza US Gendarmerie ya Niger mabao 4-0 usiku wa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Mchengerwa ametoa pongezi hizo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mpambano huo ambapo amesema ushindi huo ni ushindi wa kihistoria.
    "Ninaipongeza Timu ya Simba kwa ushindi  wa kishindo kuelekea kwenye Robo Fainali ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika. Kama Taifa, tunajivunia kwa ushindi huo mnono unaoitangaza Nchi yetu kimataifa." Amefafanua Mhe. Mchengerwa
    Ameitaka Timu ya Simba kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo hatimaye kuchukua kombe na kuendelea kuitangaza Tanzania duniani.
    Simba kwenye michuano ya robo fainali inaweza kukutana na TP Mazembe(DR Congo), Orlando Pirates ( Afrika Kusini) na Al Ahly Tripoli (Libya).
    Ukiachilia timu hizi nne(4) timu nyingine nne(4) ambazo zimefuzu kuingia robo fainali ya mashindano haya ni pamoja na RS Berkane (Morocco), Pyramids (Misri), Al-Ittihad (Libya) na Al Masry Misri.
    Simba inatarajiwa kuanzia nyumbani Uwanja wa Mkapa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAIPONGEZA SIMBA SC KUTINGA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top