• HABARI MPYA

  Sunday, April 24, 2022

  BAYERN MUNICH WAWEKA REKODI MPYA YA MATAJI ULAYA


  VIGOGO, Bayern Munich wamefanikiwa kutwaa taji la 10 mfululizo la Bundesliga baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya mahasimu, Borussia Dortmund jana.
  Ushindi huo ulitokana na mabao ya Serge Gnabry, Robert Lewandowski na Jamal Musiala unaifanya Bayern itawe ubingwa kwa tofauti ya pointi 12 na Dortmund wanaofuatia na huo ni ushindi wa nane mfululizo dhidi ya Dortmund kwenye ligi ambao hawajashinda mechi yoyote Munich tangu mwaka 2014.
  Na taji hilo la 10 mfululizo kwa Bayern ni rekodi katika ligi kubwa tano Ulaya, wakifuatiwa Juventus iliyowahi kubeba mataji tisa mfululizo ya Serie A kuanzia msimu wa 2012- hadi 2020.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH WAWEKA REKODI MPYA YA MATAJI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top