• HABARI MPYA

  Thursday, April 14, 2022

  FIRMINO AIPELEKA LIVERPOOL NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA


  WENYEJI, Liverpool wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya sare ya 3-3 na Benfica ya Ureno usiku wa Jumatano katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Uwanja wa Anfield, Liverpool, England.
  Liverpool inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-4 kufuatia kuwachapa 2-1 Benfica kwao wiki iliyopita.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Ibrahima Konate dakika ya 21 na Roberto Firmino mawili, dakika ya 55 na 65, wakati ya Benfica yamefungwa na Goncalo Ramos dakika ya 32, Roman Yaremchuk dakika ya 73 na Darwin Nunez dakika ya 81.
  Sasa Liverpool itakutana na Villarreal ya Hispania iliyoitoa Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla la mabao 2-1, ikishinda 1-0 nyumbani na sare y 1-1 Ujerumani juzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIRMINO AIPELEKA LIVERPOOL NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top