• HABARI MPYA

  Tuesday, April 05, 2022

  NI SIMBA NA ORLANDO PIRATES ROBO FAINALI SHIRIKISHO


  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC watamenyana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Simba wataanzia nyumbani Aprili 17, kabla ya kusafiri kwenda Houghton Jijini Johannesburg kwa mchezo wa marudiano Aprili 24.
  Mechi nyingine za Robo Fainali ni baina ya timu za Libya tupu, Al-Ittihad dhidi ya Al-Ahli Tripoli,  Pyramids ya Misri dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Al-Masry ya Misri dhidi ya RS Berkane ya Morocco.
  Mechi zote za kwanza zitachezwa Aprili 17 na marudiano Aprili 24, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI SIMBA NA ORLANDO PIRATES ROBO FAINALI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top