• HABARI MPYA

  Sunday, April 03, 2022

  MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO ZAISHA KWA SARE


  MECHI zote za Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo zimemalizika kwa sare, 1-1 Mtibwa Sugar na Kagera Sugar mkoani Morogoro na 0-0 na KMC na Namungo FC Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo uliotangulia mchana, George Chota alianza kuwafungia wenyeji, Mtibwa Sugar dakika ya 37 Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, kabla ya Erick Mwijage kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 69.
  Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya 13, wakati Kagera Sugar inafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 19.
  KMC baada ya sare ya leo inafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya nane, wakati Namungo FC inatimiza pointi 26, ingawa inabaki nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 19 pia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO ZAISHA KWA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top