• HABARI MPYA

  Sunday, April 10, 2022

  MAN CITY NA LIVERPOOL SARE 2-2 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City wamelazimishwa sare ya 2-2 na wapinzani wakuu katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Kevin De Bruyne alianza kuwafungia City dakika ya tano tu akimalizia pasi ya Bernardo Silva, lakini Diogo Jota akaisawazishia Liverpool dakika ya 13 akimalizia pasi ya Trent Alexander-Arnold.
  Gabriel Jesus akaitanguliza tena Man City dakika ya 36 akimalizia pasi ya João Cancelo, kabla ya Sadio Mané kuisawazishia Liverpool dakika ya 46 akimalizia pasi ya Mohamed Salah.
  Kwa sare hiyo, Manchester City inafikisha pointi 74 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 31.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY NA LIVERPOOL SARE 2-2 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top