• HABARI MPYA

  Friday, April 29, 2022

  AZAM FC YALAZIMISHA SARE KWA GEITA, 2-2


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya 2-2 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu, Geita,
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na washambuliaji wake nyota, George Mpole dakika ya 26 na Daniel Lyanga dakika ya 82, wakati ya Azam FC yamefungwa na Ismail Aziz Kader dakika ya 35 na Chilo Mkama la kujifunga dakika ya 89.
  Azam FC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 20, sawa na Namungo waliocheza mechi moja zaidi zikifuatana nafasi ya tatu na ya nne, wakati Geita Gold sasa ina pointi 28 za mechi 21 nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHA SARE KWA GEITA, 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top