• HABARI MPYA

  Friday, April 08, 2022

  REFA KOMBA KUWACHEZESHA MAMELODI LIGI YA MABINGWA


  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemteua refa Frank Komba wa Tanzania kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha mchezo wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, baina ya wenyeji, Mamelodi Sundowns na Petro Atlètico ya Angola Aprili 24, mwaka huu Uwanja wa FNB Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.


  Kwa upande wake, Meneja Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto ameteuliwa na CAF kuwa Mratibu (General Coordinator) wa mchezo wa Robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Al-Masry SC na RS Berkane Ya Morocco Aprili 17, mwaka huu nchini Misri.


  Naye Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo ameteuliwa kuwa Ofisa Habari wa mchezo wa Robo fainali Kombe la Shirikisho baina ya wenyeji,  Simba SC na Orlando Pirates ya Afrika Kusini Aprili 17 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA KOMBA KUWACHEZESHA MAMELODI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top