• HABARI MPYA

  Friday, April 29, 2022

  MAN UNITED SARE 1-1 NA CHELSEA OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Chelsea ilitangulia kwa bao la Marcos Alonso dakika ya 60 akimalizia pasi ya Kai Havertz kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Man United dakika ya 62 akimalizia pasi ya Nemanja Matić.
  Chelsea inafikisha pointi 66 katika mchezo wa 33, ingawa inabaki nafasi ya tatu na Manchester United inatimiza pointi 57 katika mchezo wa 35, japokuwa inasalia nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED SARE 1-1 NA CHELSEA OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top