• HABARI MPYA

  Monday, April 18, 2022

  MTIBWA SUGAR YAIBAMIZA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI


  WENYEJI, Dodoma Jiji FC jana wamechapwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ dakika ya tisa na Mururi Mayanja Brian dakika ya 26, wakati bao pekee la Dodoma Jiji lilifungwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 83.
  Mtibwa Sugar inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya nne, wakati Dodoma Jiji FC wanabaki na pointi zao 21 za mechi 21 sasa nafasi ya 14.
  Katika mchezo uliotangulia Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, wenyeji Kagera Sugar walilazimishwa sare ya 0-0 na KMC.
  Kagera Sugar inafikisha pointi 26 nafasi ya tano na KMC pointi 24 nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAIBAMIZA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top