• HABARI MPYA

  Monday, April 11, 2022

  COASTAL NAYO YATINGA NUSU FAINALI ASFC KWA MATUTA


  WENYEJI, Coastal Union wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Erick Mwijage alianza kuifungia Kagera Sugar dakika ya sita, kabla ya kiungo Mcameroon, Vincent Abubakar kuisawazishia Coastal Union dakika ya 68.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL NAYO YATINGA NUSU FAINALI ASFC KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top