• HABARI MPYA

  Thursday, April 28, 2022

  LIVERPOOL YAICHAPA VILLARREAL 2-0 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Villarreal ya Hispania katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield, Liverpool.
  Bao kwanza la Liverpool beki wa Kimataifa wa Ecuador, Pervis Josué Estupiñán Tenorio alijifunga dakika ya 53 akijaribu kuokoa krosi ya Jordan Henderson. 
  Na la pili lilifungwa na mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mané dakika mbili tu baadaye akimalizia pasi ya nyota wa Misri, Mohamed Salah na sasa timu hizo zitarudiana  Mei 3 Uwanja wa De la Cerámica mjini Villarreal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA VILLARREAL 2-0 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top