• HABARI MPYA

  Monday, April 25, 2022

  SIMBA SC YAFA KIUME, YATOLEWA KWA MATUTA SAUZI

  KWA mara nyingine tena, safari ya Simba katika michuano ya Afrika imeishia kwenye Robo Fainali baada ya kutolewa na Orlando Pirates katika Kombe la Shirikisho leo kwa penalti 4-3.
  Orlando Pirates walimaliza dakika 90 wakishinda 1-0 Uwanja wa Orlando Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, bao la Peprah Kwame dakika ya 60 kwa kichwa, hivyo kufanya sare ya jumla ya 1-1 baada ya Simba kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya Robo Fainali wiki iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Kwenye mikwaju ya penalti Jonás Mkude na Hennock Inonga Baka walikosa upande tea Simba, huku Shomari Kapombe, Meddie Kagere na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wakifunga.
  Waliofunga penalti za Orlando Piratas ni Deon Hotto, Hellings ‘Gabadinho’ Mhango, Tshegofatso Mabasa na kipa Richard Ofori , huku ya Kabelo Dlamini ikiokolewa na kipa Aishi Manula.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAFA KIUME, YATOLEWA KWA MATUTA SAUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top