• HABARI MPYA

  Sunday, April 17, 2022

  SIMBA SC YATANGULIZA KIFUA NUSU FAINALI SHIRIKISHO  WENYEJI, Simba SC wametanguliza kifua Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la Simba inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin limefungwa na beki mkongwe wa kulia, Shimari Salum Kapombe kwa penalti dakika ya 68.
  Penalti hiyo ilitolewa na refa Mtunisia, Haythem Guirat aada ya winga Mghana, Bernard Morrison kwenye boksi.
  Timu hizo zitarudiana Jumapili ijayo Uwanja wa Orlando Jijini Johannesburg.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATANGULIZA KIFUA NUSU FAINALI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top