• HABARI MPYA

  Thursday, April 07, 2022

  SIMBA YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 MKWAKWANI


  MABINGWA watetezi, Simba SC wamepata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mghana, Bernard Morrison dakika ya 40 na mshambuliaji Mnyarwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 90 na ushei, wakati la Coastal Union limefungwa na mshambuliaji Mnigeria, Victor Patrick Akpan dakika ya 78.
  Simba inafikisha pointi 40 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 18, ingawa inabaki nafasi ya pili ilizidiwa pointi 11 na watani, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
  Coastal Union baada ya ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 21 za mechi 19 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top