• HABARI MPYA

  Friday, April 08, 2022

  BARCELONA YATOA SARE 1-1 NA FRANKFURT UJERUMANI


  WENYEJI, Eintracht Frankfurt jana wamelazimishwa sare ya 1-1 na Barcelona katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya UEFA Europa League Uwanja wa Deutsche Bank Park Jijini Frankfurt, Ujerumani.
  Frankfurt walitangulia kwa bao la Ansgar Knauff dakika ya 48, kabla ya Ferran Torres kuisawazishia Barca dakika ya 66.
  Timu hizo mbili zilizoqngukia kwenye michuano hiyo kutoka Ligi ya Mabingwa, zitarudiana Aprili 14 Hispania na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya West Ham United ya England na Lyon ya  Ufaransa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA YATOA SARE 1-1 NA FRANKFURT UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top