• HABARI MPYA

  Monday, April 04, 2022

  WIZARA YA MICHEZO YAANZISHA TAMASHA  WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanzisha Tamasha la kimkakati la Mtaa kwa Mtaa kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa katika sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana na kuviendeleza na kutoa ajira kwa vijana nchini.
  Wizara imekuja na mkakati huo kuhakikisha nchi nzima kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa kunakuwa na uwakilishi kutoka mikoa yote nchini na hatimaye Taifa Cup ambayo itahusisha mikoa yote nchini ili kuimarisha uzalendo na uchumi miongoni mwa jamii.
  Akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo Aprili 4, 2022 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara hiyo ni ya kimkakati na ni muhimu kwa taifa ambapo amewahimiza washiriki hao kuchapa kazi kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya 2020-205, Dira ya Maendeleo ya Taifa na Miongozo ya Viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
  "Twendeni tukachape kazi, tukatangaze utamaduni wetu ili kuuendeleza kwa vijana wetu, kuongeza mapato na kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla" amesema Dkt. Abbasi.
  Akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo, Mkutugenzi wa Maendeleo ya Michezo mchini Bw. Yusuph Singo amesema dhana ya mtaa kwa mtaa katika sekta ya michezo imegawanyika katika maeneo matatu.
  Mitaa hiyo ni mtaa iliyoainishwa kwa mujibu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  mtaa wa pili unahusisha michezo katika taasisi ikiwemo UMITASHUMTA, UMISSETA, SHIMIWI, UMISEVUTA, SHIMUTA na mtaa wa tatu unajumuisha mashirikisho ya michezo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WIZARA YA MICHEZO YAANZISHA TAMASHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top