• HABARI MPYA

  Monday, April 04, 2022

  WAZIRI MKUU MGENI RASMI KIKAO CHA MAAFISA MICHEZO


  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa kesho Aprili 5, 2022 anatarajia kuwa Mgeni Rasmi kwenye kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara jijini Dodoma.
  Hayo yamesemwa leo Aprili 4, 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara. Dkt, Hassan Abbasi wakati akiwa Mwenyekiti wa kikao kazi hicho.
  Dkt Abbasi amesema kada za maafisa Utamaduni na Michezo ni kada za kimkakati kwa maendeleo ya nchi yetu.
  Aidha, amesema kikao kazi hicho kimekuja katika wakati mwafaka ambapo lugha adhimu ya kiswahili imepata msukumo mkubwa duniani na sanaa imekuwa kazi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye ajira kwa vijana.
  Kwa upande wa Michezo amesema ni wakati ambapo michezo imepiga hatua kubwa.
  Ameyataja baadhi ya mambo kuwa ni pamoja na kushiriki kwenye mashindano makubwa ya jumuiya ya madola na mashindano ya dunia ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu.
  Ametumia muda huo kuipongeza timu ya simba kwa kufuzu kuingia robo fainali ya mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika.
  Kikao hicho kinahudhuriwa pia na wataalam wa kutoka TAMISEMI na kesho wakati wa ufunguzi rasmi kitarushwa mbashara na TBC. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI MKUU MGENI RASMI KIKAO CHA MAAFISA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top