• HABARI MPYA

  Tuesday, April 12, 2022

  SIMBA NA ORLANDO KUSINDIKIZWA NA QURAN TUKUFU JUMAPILI


  MECHI ya kwanza ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC na Orlando Pirates ya Afrika Kusini itafanyika sambamba na mashindano ya Quran Jumapili ijayo.
  Hayo yamesemwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally katika mkutano wake na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam.
  “Maswali yamekuwa mengi kuhusu Uwanja wa Mkapa sababu siku ya mchezo dhidi ya Orlando Pirates kutakuwa na mashindano makubwa ya Quran, na inafahamika kwamba uwanja unatakiwa kuwa wazi kwa masaa 72 kabla ya mchezo,”.
  “Baada ya mazungumzo baina ya Simba, CAF, TFF na waandaaji wa mashindano ya Quran tumekubaliana matukio yote yatafanyika ndani ya siku hiyo moja na CAF wamebariki hilo,” amesema Ahmed Ally. 
  Mechi hiyo inatarajiwa kuanza Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na timu hizo zitarudiana Aprili 24, Uwanja wa Orlando Jijini Johannesburg.
  Msimu uliopita Simba ilitolewa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa kuifungia 4-0 Johannesburg na kushinda 3-0 Dar es Salaam, lakini safari hii Wekundu wa Msimbazi wamepania kutinga Nusu Fainali.
  “Hii ni robo fainali ya aina yake, iwe mchana iwe usiku, Mnyama safari hii anaenda semi final, tumedhamiria hilo, tumejipanga kwa hilo ndio maana tunataka mashabiki mje kwa wingi,” alisema Ahmed Ally jana.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA ORLANDO KUSINDIKIZWA NA QURAN TUKUFU JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top