• HABARI MPYA

  Sunday, April 24, 2022

  LIVERPOOL YAICHAPA EVERTON 2-0 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu, Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield, Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Andrew ‘Andy’ Robertson dakika ya 62 na Divock Origi dakika ya 85 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 79, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi moja na Manchester City baada ya wote kucheza mechi 33.
  Everton baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 29 za mechi 32 sasa nafasi ya 18 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA EVERTON 2-0 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top