• HABARI MPYA

  Friday, April 22, 2022

  POLISI TANZANIA YADAI MAKAPU ALITOROKA MECHI NA SIMBA

  UONGOZI wa klabu ya Polisi Tanzania umesema haufahamu alipo mchezaji wake, anayemudu kucheza nafasi ya beki na kiungo, Mzanzibari Said Juma Makapu.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema mchezaji huyo alitoweka kambini siku moja kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC Apriil 10, mwaka huu.
  Lukwaro amesema mchezaji huyo wa zamani wa Yanga hajawasiliana na uongozi tangu atoroke kambini, hivyo na hawafahamu alipo na juhudi za kumsaka  zinaendelea.


  Lukwaro amemtaka mchezaji huyo kurejea kambini Mara Moja na kuendelea na majukumu yake lakini pia akimtaka mchezaji huyo kueleza sababu za yeye kutoweka kambini bila ya taarifa yoyote.
  Ufafanuzi wa Lukwaro umekuja baada ya wadau wa Polisi Tz kuuhoji uongozi wa timu hiyo alipo mchezaji huyo ambaye ni mojawapo ya nguzo imara ya timu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YADAI MAKAPU ALITOROKA MECHI NA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top