• HABARI MPYA

  Sunday, April 24, 2022

  CHELSEA YAICHAPA WEST HAM 1-0 STAMFORD BRIDGE


  BAO pekee la Christian Pulisic dakika ya 90 limewapa wenyeji, Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 65 katika mchezo wa 32, ingawa inasalia nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi 14 na Liverpool na 15 na Manchester City ambao kwa pamoja wamecheza mechi 33 kila timu.
  West Ham baada ya kupoteza mechi hiyo wanabaki na pointi zao 52 za mechi 34 sasa nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAICHAPA WEST HAM 1-0 STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top