• HABARI MPYA

  Saturday, April 16, 2022

  SERENGETI GIRLS YAITANDIKA BURUNDI 4-0 URUKUNDO


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 imeibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Burundi katika mchezo wa Raundi ya Tatu Kufuzu Kombe la Dunia jioni ya leo Uwanja wa Urukundo mjini Mwumba.
  Mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Clara Luvanga dakika ya 32 na 78, Neema Kinega dakika ya 50 na Husna Mpanja dakika ya 89.
  Timu hizo zitarudiana Mei 1 Zanzibar  na mshindi wa jumla atamenyana na mshindi kati ya Zambia na Cameroon katika Raundi ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya India katika Fainali ambazo zitaanza Oktoba 11 hadi 30.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI GIRLS YAITANDIKA BURUNDI 4-0 URUKUNDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top