• HABARI MPYA

  Monday, April 18, 2022

  CHELSEA YAIFUATA LIVERPOOL FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND


  TIMU ya Chelsea imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace Jumapili Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Katika mchezo huo mkali wa Nusu Fainali, mabao ya The Blues yamefungwa na Ruben Loftus-Cheek dakika ya 65 na Mason Mount dakika ya 76.
  Sasa Chelsea watakutana na Liverpool katika Fainali Mei 14, yakiwa ni marudio ya Fainali ya Carabao Cup   ambayo Liverpool ilishinda kwa penalti 11-10 baada ya sare ya 0-0 Februari 27 hapo hapo Wembley.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAIFUATA LIVERPOOL FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top