• HABARI MPYA

  Sunday, April 24, 2022

  YANGA PRINCESS YAFUTA UTEJA KWA SIMBA QUEENS


  TIMU ya Yanga Princess imeweka historia baada ya kuibuka na ushindi kwa mara ya kwanza dhidi ya mahasimu, Simba Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la Yanga Princess katika mchezo wa leo limefungwa na Clara Luvanga dakika ya 45 na kwa ushindi huo, Watoto we Malkia wa Jangwani wanafikisha pointi 35, ingawa wanabaki nafasi ya tatu, nyuma ya Fountain Gate Princess wenye pointi 38 na mabingwa watetezi, Simba Queens wenye pointi 42 baada ya wote kucheza mechi 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA PRINCESS YAFUTA UTEJA KWA SIMBA QUEENS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top