• HABARI MPYA

  Wednesday, April 13, 2022

  AZAM FC YAICHAPA POLISI 3-0 KUTINGA NUSU FAINALI ASFC


  WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Rodgers Kola dakika ya 24, Ismail Aziz Kader dakika ya 45 na Mudathir Yahya dakika ya 78 na sasa Azam FC watamenyana na Coastal Union ya Tanga iliyoitoa Kagera Sugar.
  Timu nyingine iliyotinga Nusu Fainali ni Yanga ambayo imeitoa Geita Gold na itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho baina ya mabingwa watetezi, Simba na Pamba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA POLISI 3-0 KUTINGA NUSU FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top