• HABARI MPYA

  Friday, April 22, 2022

  MBUNI, COPCO ZAPANDA LIGI YA CHAMPIONSHIP


  TIMU ya Mbuni FC ya Arusha imefanikiwa kupanda Ligi ya Championship kutoka First League baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 katika mchezo wa Nusu Fainali leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Nayo Copco Veteran FC imepanda pia Championship baada ya ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 na Alliance FC, zote za Mwanza hapo hapo Nyamagana.
  Sasa Mbuni FC na Copco zitakutana katika Fainali ya Firts League kukamilisha msimu wa ligi hiyo ambayo ni ngazi ya tatu kwa ukubwa nchini baada ya Ligi Kuu na Championship.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBUNI, COPCO ZAPANDA LIGI YA CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top