• HABARI MPYA

  Saturday, April 16, 2022

  RONALDO APIGA HAT TRICK MAN UNITED YASHINDA 3-2


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Norwich City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao yote ya Man United leo yamefungwa na mshambuliaji Mreno, Cristiano Ronaldo dakika ya saba, 32 na 76, hiyo ikiwa hat trick yake ya 50 kihistoria, wakati ya Norwich yamefungwa na Kieran Dowell dakika ya 45 na ushei na Teemu 
  Pukki dakika ya 52.
  Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 32 na kupanda nafasi ya tano, wakati Norwich inabaki na pointi zake 21 baada ya kucheza mechi 31 pia na kuendelea kushika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APIGA HAT TRICK MAN UNITED YASHINDA 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top