• HABARI MPYA

  Monday, April 18, 2022

  HIVI NDIVYO MORRISON ALIVYOIPATIA SIMBA PENALTI YA USHINDI


  BEKI wa Orlando Pirates, Fortune Makaringe akimuangusha winga Mghana wa Simba, Bernard Morrison kwenye boksi jana katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


  Refa Mtunisia, Haythem Guirat aliamuru mkwaju wa penalti ambao uliwekwa nyavuni na beki kimataifa wa Tanzania, Shimari Salum Kapombe kuipatia bao pekee Simba katika mchezo huo.
  Timu hizo zitarudiana Jumapili ijayo Uwanja wa Orlando Pirates Jijini Johannesburg na mshindi wa jumla atakwenda Nusu Fainali.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIVI NDIVYO MORRISON ALIVYOIPATIA SIMBA PENALTI YA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top