• HABARI MPYA

    Sunday, April 24, 2022

    TYSON FURY ASTAAFU BAADA YA KUMCHAPA WHITE KO RAUNDI YA SITA


    BONDIA Tyson Luke Fury 'Gipsy King' ametangaza rasmi kustaafu ndondi baada ya kutetea tena taji lake la WBC uzito wa juu kwa kumpiga Muingereza mwenzake, Dillian Whyte mbele ya mashabiki 94,000 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
    Fury alimmaliza White kwa Knockout (KO) raundi ya sita na ikibidi awekewe kifaa cha kumsaidia kupumua baada ya kichapo hicho.
    Fury anastaafu baada ya kushinda mapambano 
    Anakuwa bondia wa pili tu wa uzito wa juu baada ya Mmarakani, marehemu Rocco Francis Marchegiano 'Rocky Marciano' kustaafu bila kupoteza pambano.
    Marciano aliyepigana ngumi za kulipwa kuanzia mwaka 1947 hadi 1955, alishikilia ubingwa wa dunia kuanzia mwaka 1952 hadi 1956 kabla ya mbabe huyo aliyekuwa anapigana style ya Orthodox kama Fury kufariki dunia Agosti 31, mwaka 1969 akiwa ana umri wa miaka 45 huko Newton, Iowa, Marekani.


    Alipigana jumla ya mapambano 49 akishinda yote, 43 kati ya hayo kwa KO, wakati Fury ameshinda mapambano 32, kati ya hayo, 23 kwa KO na amedroo pambano moja.
    Lakini Fury ambaye awali alishikilia mataji ya WBA (Super), IBF, WBO, IBO na The Ring baada ya kumpiga Wladimir Klitschko mwaka 2015, anastaafu wakati bado wapenzi wa ngumi wana hamu ya kumuona akipigana na Muingereza mwenzake mwingine, Anthony Joshua, bingwa wa zamani wa dunia pia.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TYSON FURY ASTAAFU BAADA YA KUMCHAPA WHITE KO RAUNDI YA SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top