• HABARI MPYA

  Friday, April 22, 2022

  FEI TOTO NA AUCHO FITI KABISA KUIVAA NAMUNGO KESHO


  KIUNGO Mzanzibari wa Yanga SC, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ aliyekosekana tangu mwezi uliopita yuko fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Pamoja na Fei Toto, kiungo Mganda Khalid Aucho aliyekosekana pia tangu mwezi uliopita na winga Mkongo, Chico Ushindi nao wako tayari kwa mchezo wa kesho.
  Lakini kwa mujibu wa Kocha Msaidizi, Cedric Kaze kesho Yanga itawakosa kiungo Mrundi mwenzake, Saido Ntibanzokiza na majeruhi wa muda mrefu, mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne ataendelea kukosekana.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEI TOTO NA AUCHO FITI KABISA KUIVAA NAMUNGO KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top