• HABARI MPYA

  Tuesday, April 12, 2022

  FIFA YAIFUNGIA BIASHARA KUSAJILI, KATIBU AFUNGIWA MIAKA MITANO  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifungia klabu ya Biashara United kufanya usajili wa wachezaji wapya kuanzia dirisha dogo la Januari 2022 kwa kushindwa kumlipa mishahara mchezaji wake, Timoth Omwenga.
  Beki huyo Mkenya alipeleka malalamiko yake FIFA na Biashara ikazuiwa kufanya usajili mpya hadi imalizane naye, lakini uongozi wa Klabu hiyo ukakaidi agizo hilo.
  Hiyo imemponza Katibu wa Biashara United, Hajji Mtete kufungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIFA YAIFUNGIA BIASHARA KUSAJILI, KATIBU AFUNGIWA MIAKA MITANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top