• HABARI MPYA

  Monday, April 04, 2022

  PRISONS YAZINDUKA, YAICHAPA DODOMA JIJI 3-2 SOKOINE


  WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Jumanne Elfadhili dakika ya 18 na Benjamin Asukile dakika ya 78 na 90 na ushei, wakati ya Dodoma Jiji yamefungwa na Anuary Jabir dakika ya sita na Salmin Hoza dakika ya 32.
  Kwa ushindi huo, Prisons wanafikisha pointi 16 na kusogea nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, wakati Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao 21, nafasi ya 12 baada ya timu zote kucheza mechi 19.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kusalia Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAZINDUKA, YAICHAPA DODOMA JIJI 3-2 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top