• HABARI MPYA

  Wednesday, April 27, 2022

  MAN CITY YAICHAPA REAL MADRID 4-3 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City jana wamepata ushindi wa 4-3 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad, Jijini Manchester.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ya pili, Gabriel Jesus dakika ya 11, Phil Foden dakika ya 53 na Bernardo Silva dakika ya 74.
  Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 33 akimalizia pasi ya Mfaransa mwenzake, beki Ferland Mendy dakika ya 33 na la penalti ya Panenka dakika ya 82 na lingine Vinícius Júnior dakika ya 55.
  Timu hizo zitarudiana Mei 4 Uwanja wa Santiago Bernabeu Jijini Madrid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA REAL MADRID 4-3 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top