• HABARI MPYA

  Sunday, April 10, 2022

  YANGA YAENDA KUISUBIRI SIMBA NUSU FAINALI ASFC


  VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalti 7-6 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Geita Gold walitangulia kwa bao la Offen Chikola dakika ya 87, kabla ya Yanga kusawazisha kwa bao la mkwaju wa penalti wa beki Mkongo, Djuma Shabani dakika ya 90 na ushei.
  Waliofunga penalti za Yanga ni Saido Ntibanzokiza, Yanick Bangala, Fiston Kalala Mayele, Jesus Moloko, Djuma Shabani, Bakari Mwanyeto na Dickson Job, wakati kipa Djigui Diarra alipiga nje.
  Upande wa Geita Gold waliofunga ni Yussuf Kagoma, George Mpole, David Kameta ’Duchu’, Adeyoum Ahmed, Offen Chikola na Kelvin Yondan, wakati wachezaji wawili wa zamani wa Yanga, viungo wote walikosa, Maka Edward iligonga mwamba na Juma Mahadhi ilifikia mikononi mwa kipa Diarra.
  Sasa Yanga itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na Pamba FC ya Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAENDA KUISUBIRI SIMBA NUSU FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top