• HABARI MPYA

  Wednesday, April 13, 2022

  BENZEMA AIPELEKA REAL NUSU FAINALI, BAYERN OUT


  WENYEJI, Real Madrid wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuchapwa mabao 3-2 na waliokuwa mabingwa watetezi, Chelsea usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid, Hispania.
  Mabao ya Chelsea yalifungwa na Mason Mount dakika ya 15, Antonio Rudiger dakika ya 51 na Timo Werner dakika ya 75, wakati ya Real Madrid yalifungwa na Rodrygo dakika ya 80 na Karim Benzema dakika ya 96.
  Baada ya The Blues kumaliza wanaongoza 3-1, mechi iliongezewa dakika 30, kwa sababu matokeo ya jumla yalikuwa 4-4.
  Real wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-4 baada ya kuwachapa mabingwa hao wa msimu uliopita 3-1 kwenye mechi ya kwanza Jumatano iliyopita Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mechi nyingine ya jana, wenyeji Bayern Munich wametupwa nje baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Villarreal, hivyo kutupwa nje kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia kuchapwa 1-0 Hispania kwenye mechi ya kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENZEMA AIPELEKA REAL NUSU FAINALI, BAYERN OUT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top