• HABARI MPYA

  Sunday, April 10, 2022

  CHELSEA YAWATANDIKA SOUTHAMPTON 6-0 ST MARY’S


  TIMU ya Chelsea imezinduka kwa ushindi wa 6-0 dhidi ya wenyeji, Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. Mary's, Southampton, Hampshire.
  Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na Marcos Alonso dakika ya nane, Mason Mount dakika ya 16 na 54, Timo Werner dakika ya 21 na 49 na Kai Havertz dakika ya 31.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 59 katika mchezo wa 29, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi 13 na Liverpool walio nafasi ya pili, nyuma ya Manchester City wenye pointi moja zaidi yao, wote wakiwa wamecheza mechi 30.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAWATANDIKA SOUTHAMPTON 6-0 ST MARY’S Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top