• HABARI MPYA

  Friday, April 22, 2022

  TAIFA STARS KUANZIA NIGER KUMALIZIA ALGERIA KUFUZU AFCON 2023


  TANZANIA itaanzia ugenini dhidi ya Niger kati ya Mei 30 na Juni 14 katika mechi za Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast.
  Mechi ya pili, Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Algeria Jijini Dar es Salaam kati ya Mei 30 na Juni 14, kabla ya kuifuata Uganda kwa mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza kati ya Septemba 19 na 27 Jijini Kampala.
  Mechi za mzunguko wa pili Taifa Stars itaanzia nyumbani dhidi ya Uganda kati ya Septemba 19 na 27, kabla ya kuwakaribisha Niger kati ya Machi 20 na 28 mwakani, kisha kwenda kukamilisha mechi zake za kuwania tiketi ya Ivory Coast 2023 kwa kumenyana na Algeria - bila shaka mjini Blida kati ya Machi 20 na 28 mwakani.
  Timu mbili za juu zitafuzu moja kwa moja fainali hizo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS KUANZIA NIGER KUMALIZIA ALGERIA KUFUZU AFCON 2023 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top