• HABARI MPYA

  Sunday, April 17, 2022

  MANE AIPELEKA LIVERPOOL FAUNALI FA, CITY YAFA 3-2 WEMBLEY


  TIMU ya Liverpool imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester City leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na beki Mfaransa, Ibrahima Konaté dakika ya tisa na mshambuliaji Msenegal, Sadio Mane dakika ya 17 na 45, wakati ya Man City yamefungwa na Jack Grealish dakika ya 47 na Bernardo Silva dakika ya 12 ya muda wa fidia baada ya kutimia dakika 90 za kawaida.
  Sasa Liverpool itamenyana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili Jumapili baina ya Chelsea Crystal Palace katika Fainali itakayofanyika Mei 14 hapo hapo Wembley.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANE AIPELEKA LIVERPOOL FAUNALI FA, CITY YAFA 3-2 WEMBLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top