• HABARI MPYA

  Sunday, April 10, 2022

  SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE NA POLISI 0-0 MOSHI


  MABINGWA watetezi, Simba SC wamelazimishwa sare ya bila mabao na wenyeji, Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Kwa sare hiyo inayoiongezea kila timu pointi moja, Simba inafikisha pointi 41 na wanabaki nafasi ya pili, wakizidiwa pointi 10 na watani wao wa jadi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 19.
  Polisi Tanzania inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 19 pia na kusogea kwa nafasi moja hadi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE NA POLISI 0-0 MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top