• HABARI MPYA

  Friday, April 15, 2022

  BARCELONA YAPIGWA 3-2 CAMP NOU NA KUTUPWA MJE EUROPA LEAGUE


  WENYEJI, Barcelona wametupwa nje UEFA Europa League baada ya kuchapwa 3-2 na Eintracht Frankurt ya Ujerumani usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou, Barcelona nchini Hispania.
  Mabao ya Eintracht Frankurt yalifungwa na Filip Kostic mawili dakika ya nne kwa penalti na 69 na Santos Borre dakika ya 36, wakati ya Barca yalifungwa na Sergio Busquets dakika ya 90 na ushei na Memphis Depay kwa penalti dakika ya ushei pia.
  Kwa matokeo hayo, Eintracht Frankurt wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-3 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Ujerumani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA YAPIGWA 3-2 CAMP NOU NA KUTUPWA MJE EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top