• HABARI MPYA

  Saturday, April 23, 2022

  JESUS APIGA NNE, MAN CITY YAITANDIKA WATFORD 5-1


  WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Pongezi kwa Gabriel Jesus aliyefunga mabao manne peke yake dakika za nne, 23, la penalti dakika ya 49 na 53, wakati lingine limefungwa na Rodri dakika ya 34, huku bao pekee la Watford likifungwa na Hassane Kamara dakika ya 28.
  Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 80 katika mchezo wa 33 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.
  Watford baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 22 za mechi 33 nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JESUS APIGA NNE, MAN CITY YAITANDIKA WATFORD 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top