• HABARI MPYA

  Monday, April 18, 2022

  NAMUNGO YAICHAPA RUVU 3-1 ILULU


  WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na David Molinga ‘Falcao’ dakika ya 11, Hashim Manyanya dakika 35 na Emmanuel Charles dakika ya 88, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Saadat Mohamed dakika ya 64.
  Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 20 na kupanda nafasi ya tatu, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 21 za mechi 20 pia nafasi y 12.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao la Oscar Paul dakika ya saba limeipa Tanzania Prisons limeipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Prisons inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya 15, ikiizidi pointi Mbeya Kwanza baada ya wote kucheza mechi 20.
  Ikumbukwe mwishoni mwa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO YAICHAPA RUVU 3-1 ILULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top