• HABARI MPYA

  Tuesday, April 05, 2022

  ARSENAL YACHAKAZWA 3-0 NA CRYSTAL PALACE LONDON


  WENYEJI, Crystal Palace wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Mabao ya Crystal Palace yamefungwa na Jean-Philippe Mateta dakika ya 16, Jordan Ayew dakika ya 24 na Wilfried Zaha dakika ya 74 kwa penalti.
  Kwa ushindi huo, Crystal Palace ya kocha Patrick Vieira, Nahodha na kiungo wa zamani wa Arsenal, inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 30 nafasi ya tisa, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 54 za mechi 29 sasa nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YACHAKAZWA 3-0 NA CRYSTAL PALACE LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top