• HABARI MPYA

  Sunday, April 03, 2022

  MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE NA LEICESTER 1-1


  WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya 1-1 na Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Old Trafford, Manchester.
  The Foxes walitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Kimataifa wa Nigeria, Kelechi Iheanacho dakika ya 63, kabla ya kiungo Mbrazil, kuisawazishia Man Unitef dakika ya 66.
  Leicester ingeweza kuondoka na pointi zote tatu kama si bao Lao lingine baadaye lililofungwa na James Maddison kukataliwa kwa msaada wa VAR.
  Kwa sare hiyo, United inafikisha pointi 51 katika mchezo wa 30, ingawa inabaki nafasi ya sita, wakati Leicester inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 28 nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE NA LEICESTER 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top